[caption id="attachment_38762" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Wawakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja.[/caption] [caption id="attachment_38764" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.[/caption] [caption id="attachment_38763" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa huo wa Kiliamnjaro.[/caption] [caption id="attachment_38761" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA kwa mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo ambaye alikataa rushwa ya Dola za kimarekani $2000. Rais Dkt. Magufuli ameagizwa kuandikiwa barua ya kupongezwa kwa Meneja huyo.[/caption] [caption id="attachment_38765" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.[/caption]