Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Magangha Aongoza Kikao cha Mradi wa Kimazingira
Sep 30, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika mipango ya nchi.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Septemba 30, 2022 kimehusisha Wajumbe kutoka Wizara za kisekta, sekta binafsi na Asasi za Kiraia

Lengo la mradi huo ni kuimarisha uwezo wa nchi katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kujumuisha, masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika mipango ya maendeleo.

Mradi utawezesha wizara na taasisi kuwa na mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha uratibu wa taasisi na wadau husika katika kutekeleza mipango ya uhimilivu na maendeleo ili kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka katika sekta zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, matokeo tarajiwa ya utekelezaji wa mradi yanatarajiwa kuwa ni kuboresha uwezo wa kitaifa wa upangaji wa mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarika kwa uratibu wa taasisi na wadau.

Pia kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka katika sekta zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi pamoja na Mpango wa Taifa wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kuandaliwa na kupitishwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi