Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Maganga Akutana na Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
Jan 10, 2024
Katibu Mkuu Maganga Akutana na Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akizungumza na Ujumbe wa Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) ukiongozwa na Meneja wa GCF Kanda ya Afrika, Bi. Chihenyo Kangara katika kikao kilichofanyika ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais (

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga ameushukuru Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali nchini.

 

Ametoa shukrani hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Sekretarieti ya Mfuko huo ukiongozwa na Meneja wa GCF Kanda ya Afrika, Bi. Chihenyo Kangara katika ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.

 

Miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na GCF kwa sasa ni pamoja na Mradi wa Maji unaotekelezwa mkoani Simiyu, Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi mkoani Kigoma, Mradi wa Uandaaji wa Mpango Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na Mradi wa Kilimo kupitia benki ya CRDB.

 

Pia, Katibu Mkuu Maganga amesisitiza kuhusu umuhimu wa Taasisi za Tanzania kupata ithibati chini ya Mfuko huo na ukamilishwaji wa mapendekezo ya miradi yaliyowasilishwa GCF Ili kuwezesha upatikanaji fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati. 

 

Aidha, miradi iliyowasilishwa GCF inahusu Uchumi wa Buluu, Afya, Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia joto ardhi, Mradi wa Mabasi ya Mwendo kasi na Mradi ya Maji.

 

Kwa upande wa kiongozi wa msafara wa GCF, Bi. Chihenyo ameahidi kuhakikisha kuwa hakuna ucheleweshaji tena katika maombi mengine. 

 

Ameeleza kuwa kwa sasa wako kwenye mageuzi katika maeneo ya uongozi na mipango pamoja na taratibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea wadau ili kutoa huduma inayokubalika.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi