[caption id="attachment_46879" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzaznia (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) kuhusu kutua kwa Meli kubwa ya mizigo ya MV Grand Duke kwenye gati jipya namba sifuri katika Bandari ya Dar es Salaam[/caption]
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezikaribisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kutumia bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati namba sifuri kuanza kupokea mizigo.
Akizungmza Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo ya Magari ya kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke iliyotua bandarini hapo, Waziri Kamwelwe alifurahishwa kuona meli hiyo kubwa nyenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetia nanga ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari kupokea mizigo mikubwa.
“Tuko hapa kuwahabarisha Watanzania, na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), kwamba ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam unaenda vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa gati namba moja, mbili na hili gati namba sifuri liko mwishoni na limeanza kupokea meli kubwa za Mizigo kama mnavyoona hapo, hiyo ni meli ya mizigo ya magari yenye uwezo mkubwa sana”, Waziri Kamwelwe.
[caption id="attachment_46880" align="aligncenter" width="750"] Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)wakiongoza baadhi ya magari kutoka kawenye meli kubwa ya mizigo ya magari MV Grand Duke baada ya kutua hapo jana kwenye gati jipya namba 0 ya Bandari ya Dar es Salaam.[/caption]Malengo ya Serikali ni kufanya ukarabati wamagati nane ambapo mpaka sasa gati namba moja na gati namba mbili yako kwenye matumizi mara baada ya kukamilika na sasa meli zinaendelea kutoa huduma kama kawaida, gati namba sifuri ambalo ni maalum kwa meli za mizigo ya magari linaendelea na ukarabati lakini asilimia kubwa liko vizuri.
Waziri Kamwelwe alisema kuwa mara baada ya gati hilo kukamilika Tanzania itakuwa na uwezo mkubwa wa kupokea mizigo ya magari laki 6 kwa mwaka, lakini pia bandari hiyo inabeba tani milioni 17 kwa mwaka huku malengo ya Serikali ikiwa ni kufikia tani milioni 25 ifikapo mwaka 2021.
“Malengo yetu ni kufikia tani milioni 25 kwa mwaka tofauti na tani za sasa milioni 17, kwa hiyo Nchi Wanachama wa SADC, bandari hii sasa inafanya kazi vizuri, kwa hiyo majirani zetu kutoka SADC, DRC, Malawi, Zambia na nchi zingine za ukanda huu wa Kusini mwa Afrika wanakaribishwa sana kutumia bandari ya Dar es Salaam” Alisisitiza Waziri Kamwelwe.
[caption id="attachment_46881" align="aligncenter" width="750"] Gari likitoka kwenye meli kubwa ya mizigo ya magari MV Grand Duke baada ya kutua hapo jana kwenye gati jipya namba sifuri ya Bandari ya Dar es Salaam.[/caption]Waziri Kamwelwe alisema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kutoka Nchi Wananchama wa SADC ili maeneo ambayo yana changamoto ziweze kutatuliwa haraka.
“Serikali imewekeza fedha nyingi katika ukarabati huo, kwa hiyo itahakikisha kuwa inaipa bandari hii mizigo ya kutosha na hasa kutoka kwa Nchi Wanachama wa SADC, ili kuwawezesha kupata huduma rahisi za usafirishaji” alisema Kamwelwe
kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, alisema kuwa gati jipya namba sufuri limeanza kufanya kazi kwa kupokea meli kubwa ya Mv Grand Duke ambayo imetua jana na mzigo wa magari 1347.
[caption id="attachment_46883" align="aligncenter" width="750"] Meli kubwa ya mizigo ya magari MV Grand Duke ikiwa katika bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kutia nanga kwenye gati jipya namba sifuri la Bandari hiyo ambalo ukarabati wake unaelekea kukamilika[/caption]“ Hili gati ni Jipya ni kati ya magati nane ambayo yanajengwa, lenyewe limejengwa kwa zege kama mnavyoona, lina uwezo wa kubeba magari 10,000 kwa wakati mmoja kutoka uwezo wa kubeba magari 2,500 ambao tulikuwa nao hapo mwanzo, lakini pia lina urefu wa mita 320 kwa hiyo ni gati kubwa na hii meli ina urafu wa mita 200 kwa hiyo kuna mita 120 zimebakia kwenye gati hili”, Alisema Mhandisi Kakoko.
Gati hilo ambalo ni la kisasa Zaidi litakuwa na taa ambazo zitawezesha kufanyika kazi usiku na mchana hapo bandarini, na makabidhiano ya gati hilo yatafanyika kesho ambapo Mkandarasi ataikabidhi Mamlaka ya Bandari (TPA).
Aidha, Mhandisi Kakoko alisema kuwa meli ya Abiria ziwa nyasa imeingia kwenye majaribio ya mwezi mmoja ambapo mwezi ujao inatarajiwa kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili kuanza kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.