Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kampuni ya Shanghai Electric Yatarajia Kuwekeza Kinyerezi III.
Dec 06, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24240" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati wizara ya Nishati, James Andilile (wa pili kulia) akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kati ya Kampuni ya Shanghai Electricity. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka. Wengine katika picha ni Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).[/caption]

Na Rhoda James

Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua leo tarehe 5 Decemba, 2017 amekutana na Ujumbe kutoka Kampuni ya Shanghai Electric kutoka China katika Ofisi ya Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ili kujadili utekelezaji wa mradi huo kwa utaratibu wa EPC plus Financing. Kampuni ya Shanghai Electric itaratibu upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi huo pamoja na ujenzi wa mitambo ya kufua Megawati 600 kwa kutumia Gesi Asilia. Katika kikao hicho baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kusaini Mkataba wa Awali wa Makubaliano (MoU) kwa ajili ya Utekelezaji wa Mradi huo.

[caption id="attachment_24241" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka (wa kwanza kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania na Ujumbe kutoka Kampuni ya Shanghai Electric.[/caption] [caption id="attachment_24242" align="aligncenter" width="750"] Ujumbe kutoka Kampuni ya Shanghai Electric wakiwa katika kikao baina yao na Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi