Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu
(kulia) akipokea Salamu ya Heshima kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Muhsin A. Muhsin akimkaribisha rasmi
Kamishna huyo kutembelea Kituo cha Uhamiaji kilichopo Bandari ya Mkokotoni, Wilaya
ya Kaskazini “A” jana tarehe 06 Disemba, 2017 wakati akiendelea na ziara ya
kikazi Mkoani Humo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu
(juu) akiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja,
kuzingatia Maadili ya kazi, Heshima na Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi
uliotukuka. Pia alikemea vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya
watumishi wasio waadilifu. Alitoa nasaha hizo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati
akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin na kushoto
ni Afisa Utumishi, Mrakibu wa Uhamiaji, Ali J. Abdulkadir.
Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A.
Muhsin akiwasilisha kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, taarifa
ya utendaji kazi wa Ofisi hiyo kuanzia Julai hadi Novemba, 2017. Huku akitilia
mkazo ongezeko la makusanyo ya maduhuli ya Serikali kwa kipindi hicho, Dola za Kimarekani 34,000$ zilikusanywa.
Alitoa taarifa hiyo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati Kamishna Sururu akihitimisha
ziara ya siku tatu Mkoani Humo.
Koplo wa Uhamiaji, Mosi Shadhil Khatib akichangia hoja
zilizojadiliwa katika Kikao cha pamoja cha wafanyakazi wote wa Uhamiaji Mkoa wa
Kaskazini Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Leo tarehe
07 Disemba, 2017 wakati alihitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani humo.
Mkuu wa Bandari ya Mkokotoni, Bwana Ahmed Salim Said,
akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zaznibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa
aliombatana nao eneo linalotumiwa na baadhi ya Manahodha kushusha abiria
kinyume na utaratibu wa Bandari hiyo, wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye
maeneo ya utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana
tarehe 06 Disemba, 2017.
Sheha wa Shehia ya Mnarani Bwana Mdungi Sharifu
Makemi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na
Maafisa alioambatana nao eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za
uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo. Alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya
utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06
Disemba, 2017
Sheha wa Shehia ya Nungwi – Banda Kuu Bwana Mohamed
Khamis Haji, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na
Maafisa alioambatana nao eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za
uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo. Alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya
utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06
Disemba, 2017
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu
(kulia) akimsikiliza kwa makini Sheha wa Shehia ya Kilindi Bwana Omar Ali
Mussa (wa pili kushoto), akitoa shukran zake kwa Uongozi wa Idara kwa
ushirikiano mkubwa anaoupata toka kwa Askari wa Uhamiaji. Akisisitiza kauli
hiyo Sheha alisema “Ziara yako Kamishna imethibitisha kauli yangu na umeonesha
kwa vitendo jinsi ulivyojipanga kushirikiana na wananchi wa eneo letu kutatua
changamoto za baadhi wageni wanaoishi hapa bila ya kufata utaratibu” aliyasema
hayo jana wakati Kamishna akiendelea na ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini
Unguja.