Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Akutana na Kamishna Jenerali wa Magereza
Jul 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33619" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye ametembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.

Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.

 “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.

[caption id="attachment_33618" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi