Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Yakutana Dodoma
Oct 21, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amepokea jedwali la hoja za Kamati ya Sheria Ndogo kuhusu Sheria zilizowasilishwa katika Gazeti la Serikali katika mkutano wa (8) wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (kushoto) akipokea jedwali la hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo (kulia) Mhe. Kilumbe Ng’enda.
Mhe. Ummy amepokea jedwali hilo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kilichofanyika Oktoba 21, 2022 katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bwa. Kaspar Mmuya akieleza jambo katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Kilumbe Ng’enda akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.