Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundo Yashauri Uboreshwaji Huduma TCRA na TBC
Nov 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Paschal Dotto-MAELEZO

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na kushauri uboreshwaji wa huduma mbalimbali katika Taasisi hizo.

Akizungumza katika Mkutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), leo Novemba 14, 2022, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso, ameiomba Serikali kupitia TCRA kufanyia kazi malalamiko ya wananchi kuhusu matumizi ya bando na huduma zingine za Mawasiliano.

TCRA mnatakiwa kutoa elimu kubwa kwa Wabunge na wananchi kuhusu matumizi ya simu janja pamoja na mitandao ambapo katika huduma za ununuzi wa bando wananchi wamekuwa wakilalamika kuibiwa hela zao, lakini naamini mkitoa elimu jinsi ya kutumia mitandao malalamiko hayo yataisha, Alisema Kakoso.

Kuhusu ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Serikali ishirikishe sekta binafsi ili kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa nchi nzima hasa kwa wananchi walioko maeneo ya vijiji, lakini pia Kamati hiyo imeiomba Serikali kuhakikisha inakabidhi Mkondo wa Taifa kwa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Kakoso alisema kuwa makosa ya kimtandao ni suala ambalo ni mtambuka na inatakiwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na TCRA zishirikiane kwa pamoja ili kuondoa wizi wa kimtandao ambapo Watanzania wamekuwa wakiibiwa mara kwa mara.

Aidha, Kakoso aliipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya Mawasiliano nchini kwani kunainua uchumi kwa sasa ambapo wananchi wengi wamekuwa wakifanya biashara kupitia mitandao mbalimbali.

"Naipongeza Serikali kwa kuwekeza katika sekta hii muhimu, sekta hii ya Mawasiliano imekuwa ikitengeneza uchumi wa watu wetu lakini pia kukuza uchumi wa taifa na kuifanya nchi yetu kuwa na uchumi wa kidijitali katika sekta mbalimbali, Alisema Kakoso.

Kwa upande wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mhe. Kakoso ameiomba Serikali kuliongezea nguvu kazi ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, amesema kuwa uwekezaji uliofanyika kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Shilingi bilioni 4.1 zimetolewa kwa ajili ya marekebisho kwa TBC FM, Shirika hilo limeongeza usikivu katika maeneo mbalimbali nchini.

“TBC inafanya vizuri sana lakini inatakiwa uwekezaji wa rasilimali watu Mkurugenzi kasema hapa kuna upungufu wa watumishi 260 lakini kwa uwekezaji ambao Serikali imefanya mnaweza kuwa hata 300 kwa hiyo tafuteni vijana waje wafanye kazi hapa”Alisema Kakoso.

Naye, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Kundo Mathew ameishukuru Kamati hiyo kwa kuridhia na kupitisha Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi kwa Watanzania.

TCRA inahusika na suala ya utaoji na usimamizi wa leseni za Posta na Utangazaji nchini, lakini naomba nitoe shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu kwa kuridhia na kupitisha muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi suala hili lisingewezekana bungeni kama siyo ninyi kupitisha kwenye kamati, Alisema Mhe. Kundo Mathew.

Katika Hatua nyingine, Mhe. Kundo amesema kuwa TBC imejiimarisha kwa sababu ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika shirika hilo kufanya mageuzi ya Redio kwa kufanya ukarabati katika mwaka wa Fedha 2021/22 ambapo Shilingi bilioni 4.1 zimetumika kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza na ya pili zimekamilika na awamu ya tatu itafanyika hivi karibuni.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi