Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kaliua Kuboresha Kuboresha Yaliyokuwa Makazi ya Mtemi Milambo
Feb 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

 Na Tiganya Vicent

Uuongizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua unatarajia kuanza kuboresha makazi yalikuwa ya  Mtemi Milambo kwa ajili kuvutia wageni kutembelea eneo hilo ili kutalii na kufanya tafiti mbalimbali na hivyo kuwa chanzo kingine mapato yake na wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini Kaliua na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati akijibu hoja mbalimbali za Madiwani walitaka kujua mpango kuboresha eneo hilo kwenye Mkutano Maalumu wa kupitisha Mpango wa bajeti ya 2018/19.

Alisema lengo la kuboresha makazi hayo ni kutaka kuwepo na wageni wengi watakaotembelea hilo na hivyo kuanza kupata mapato kwa Halmashauri hiyo na wananchi kuanza kunufaika na ujio wa wageni.

Awali Diwani wa Kata ya Ilege Masanja Lufungija alisema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikikosa mapato kutokana na kutoboreshwa kwa Makazi wa Mtemi Milambo na kuthamini umuhimu wa eneo hilo.

Alisema kuwa kila wiki wageni kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi wamekuwa wakitembelea eneo hilo lakini Halmashauri hakuna kitu inachoingia kutokana na uwepo wa wageni hao.

Lufungija alisema Mtemi Milambo ni miongoni mwa viongozi ambao walikuwa na majina makubwa ndani ya Tanzania na nje na hivyo kuwavutia watu wengi kupenda kwenda kuona alipokuwa anakaa.

Alisema kuwa Halmashauri hiyo ikitumia umaarufu wake na kumuenzi kwa kuboresha eneo la yalipokuwa makazi yake ili kuongeza chanzo cha mapato.

 Naye Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu ambapo ndipo asili ya  Makazi ya Mtemi Milambo  Mhe. John Kadutu alisema kuwa eneo hilo ni vema likaboreshwa kwa kujenga hata nyumba kwa ajili ya wageni kupata huduma mbalimbali wakati wanatembelea eneo hilo kutasaidia kuongeza mapato katika Halmashauri ya Kaliua.

Jina la Milambo ni maarufu sana hapa Tanzania na katika eneo lote la ukanda wa Afrika Mashariki.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi