Zoezi la Utangazaji wa Matokeo ya Jumla ya Uchagzui wa Rais 2020, likiendeleo katika Kituo cha Mikutano kimataifa Julisu Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage, amemtangaza Dkt.John Pombe Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kura zaidi ya 12,516,252 sawa na asilimia 84.4.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza matokeo ya jumla Uchaguzi wa Rais ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli ameshinda kwa zaidi ya kura milioni 12, kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera
Wakala wa moja kati ya vyama 15 ambavyo vimeshiriki Uchaguzi wa Rais 2020 akisoma fomu ya matokeo kabla ya kuijaza katika zoezi la utangazaji wa matokeo ya jumla kwa Uchaguzi wa Rais 2020 kukamilika.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza matokeo ya jumla Uchaguzi wa Rais ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli ameshinda kwa zaidi ya kura milioni 12.
Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera akikabidhi fomu ya matokeo kwa mmoja kati ya mawakala wa vyama vilivyoshiriki Uchaguzi wa Rais 2020, ili aisome na kusaini kukubali matokeo ya Uchaguzi huo.