Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Kuendelea Kupokea Madktari Kutoka China
Aug 28, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_10644" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Madaktari kutoka China waliomaliza mikataba yao katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Naibu Mkurugenzi Gu Zhungiang na Kiongozi wa Madaktari hao Dkt. Sun Long.[/caption]

Na: Agness Moshi na Bushiri Matenda

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kusaidiana na madaktari wazawa katika taasisi hiyo baada ya madaktari wengine wanne kutoka China kumaliza muda wao.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt.Peter Kisenge katika hafla ya kuwaaga madaktari wanne kutoka China waliomaliza muda wao wa utumishi hapa nchini ambao walikua wakishirikiana naTaasisi hiyo kwa takribani miaka miwili.  

[caption id="attachment_10645" align="aligncenter" width="750"] Kiongozi wa Madaktari kutoka China Dkt. Sun Long akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Madaktari hao waliomaliza mikataba yao katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge[/caption] [caption id="attachment_10646" align="aligncenter" width="750"] Naibu Mkurugenzi wa Jopo la Madaktari kutoka China, Bw. Gu Zhungiang akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Madaktari kutoka China waliomaliza muda wa kufanyakazi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge na Kiongozi wa Madaktari hao Dkt. Sun Long (katikati).[/caption]

“Wanarudi nchini China baada ya kumaliza muda wao, Tunawashukuru kwa kushirikiana nasi kwa kipindi chote walichokua nasi tunaishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali wanayotupatia ikiwemo ujenzi wa jengo la Taasisi ya Moyo, madaktari,wataalam pamoja na vifaa tiba”, alisema Dkt.Kisenge.

Dkt.Kisenge aliongeza kuwa hivi karibuni Taasisi inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kushirikiana nao   katika utoaji huduma ili kuweza kuifanya Taasisi hiyo ya kimataifa.

Naye Kiongozi wa timu ya Madaktari kutoka China kwa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt.Sun Long amesema kwa miaka miwili waliyofanya kazi na Taasisi hiyo wamefanikiwa kufanya oparesheni  takribani 373 jambo ambalo limesaidia kupunguza  gharama za matibabu na idadi ya wagonjwa wa Moyo kwenda kutibiwa nje ya Nchi kama vile India.

[caption id="attachment_10648" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari kutoka China waliomaliza muda wao leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_10651" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi wa Jopo la Madaktari kutoka China, Bw. Gu Zhungiang wakati wa hafla ya kuwaaga madaktari waliomaliza muda wakufanyakazi katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO.)[/caption]  

“Sasa hakuna haja ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ya Moyo, Matibabu yote yanapatikana katika taasisi hii, hakuna Matata, Hapakazi Tu”, alisisitiza Dkt. Long.

Aidha, Dkt.Long amesema kuna haja ya nchi hizi mbili kuendelea kushirikiana ili kuendelea kusaidiana katika utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kubadilishana wataalam ili kukuza uwezo katika utoaji huduma.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa jopo la madaktari waliomaliza muda wao Dkt. Gu Zhigiang ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujitegemea katika matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa wananchi wake na ameshukuru ushirikiano walioupata kutoka kwa taasisi hiyo kwa kipindi chote walichofanya kazi hapa nchini.

“Ninamshuru kila mmoja na ninafurahi kuhudumia Nchi hii nzuri, ninatumaini tutaendelea kushirikiana zaidi”, alisema Dkt. Gu Zhigiang.

Dkt. Gu Zhigiang ameongeza kuwa anatarajia kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwani tunaelekea kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi