Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JK Afurahishwa na Idadi ya Wanawake Wahitimu UDSM
Oct 17, 2023
JK Afurahishwa na Idadi ya Wanawake Wahitimu UDSM
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kuhitimisha Duru la Pili la Mahafali ya 53 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Alhamisi Oktoba 17, 2023
Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefurahishwa kuona takwimu ya wahitimu wanawake chuoni hapo imefikia asilimia 54.7 na kuwashauri wanafunzi wanaume wafanye juhudi ili wasiachwe mbali sana na wenzao.

 

Akiongea kabla ya kuhitimisha Duru la Pili la Mahafali ya 53 ya chuo hicho, Dkt. Kikwete amesema kwamba kafurahishwa kuona wanawake siku hizi “wakiupiga mwingi” na kuwataka vijana wa kiume walichukulie jambo hilo kama changamoto kwao ya kufanya vizuri zaidi kwenye masomo.

 

Katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jumla ya wahitimu 2,796 walihudhurishwa ambapo 2,700 walitunukiwa Shahada za Awali ikiwa ni wasichana 1,488 na wavulana 1,212.

 

Jumla ya Stashahada 78 zilitolewa kwa wanaume 45 na wanawake 33, wakati wanaume 10 na wasichana wanane walitunukiwa Astashahada.

 

Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa William A.L. Anangisye aliwapongeza wahitimu wote huku akiwashauri watumie elimu waliyopata kuleta ushawishi chanya kwa watu wote wanaowazunguka na kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

 

Profesa Anangisye aliwaasa wahitimu hao kwamba elimu waliyoipata ni mali ya umma na kwa mantiki hiyo ni lazima ilete faida kwa umma wa Watanzania.

 

“Elimu haiwezi kuleta faida na kuwa chachu ya mabadiliko yaliyokusudiwa endapo kama haitatumika katika kutatua matatizo ya jamii”, alisema Profesa Anangisye.

 

Makamu Mkuu huyo wa chuo aliendelea kushauri: “Endapo ajira serikalini au katika sekta binafsi zitachelewa kupatikana kuweni wepesi kuangalia sehemu nyingine ambapo maarifa na ujuzi wenu unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi”. Alimalizia 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi