Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jeshi la Zimamoto Lafanya Tamasha la Utoaji Elimu kwa Umma
Dec 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25527" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Katikati), akizungusha king’ora kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Thobias Andengenye, wakati wa Tamasha la hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema jana asubuhi.[/caption]

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini limefanya Tamasha la utoaji elimu ya Kinga na Tahadhali dhidi ya majanga ya moto na majanga mengine katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi na Kiserikali pamoja na Wananchi.

Tamasha hilo ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali yakiwemo makampuni, taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali, shule za msingi na sekondari wanamichezo, wasanii, vyombo vya habari na wadau wengine.

[caption id="attachment_25528" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza na Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa Umma, wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi[/caption] [caption id="attachment_25529" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Watatu Kulia), akiwa kwenye banda la mmoja wa mdau aliyeshiriki katika tamasha hilo, wakati wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa umma lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi[/caption]

Akizungumza wakati wa Tamasha hilo, Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Billy Mwakatage alisema lengo kuu la tamasha hili ni kutoa elimu na kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya namba yetu ya dharura 114 inayotumika kutolea taarifa pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali.

Kauli mbiu ya tamasha hili ni “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa kupunguza Majanga mbalimbali, piga simu 114”

Mwakatage alisema “niwatoe hofu wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza hapa nchini kuwa, Jeshi letu limejipanga na linavifaa vya kisasa katika kukabiliana na majanga ya moto na majanga mengine kwa kuzingatia kauli mbiu ya Serikali kuwekeza kwenye viwanda”

[caption id="attachment_25530" align="aligncenter" width="750"] Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mrakibu wa Zimamoto Peter Mabusi (wanne kushoto) akitoa maelezo kwa Kamishna wa Operesheni Billy Mwakatage (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benedict Kitalika (Wapili Kushoto), na Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Temeke Laizer Loshpy (kushoto), pindi vikosi mbalimbali vya zimamoto vilivyokuwa vikioonesha zoezi la utayari wakati wa tamasha la Zimamoto na Uokoaji la utoaji elimu lililofanyika katika viwanja vya Kawe Tanganyika Packers mapema mapema jana asubuhi[/caption] [caption id="attachment_25531" align="aligncenter" width="750"] Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini wakionesha utayari wakukabiliana na majanga ya moto. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)[/caption]

Naye Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Peter Mabusi, amewataka Wanachi wa Jiji la Dar es Salaam kutembelea viwanja hivyo ili waweze kupata elimu na kuona ni jinsi gani Jeshi lao lilivyo na uwezo mkubwa wa kupambana na majanga mbalimbali.

Pia alisema “nawaomba Wananchi waweze kujitokeza kwa wingi viwanjani hapa kesho tarehe 23/12/2017 ambapo kutakuwa ni kilele cha Tamasha hili na litafungwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali”. Ufungaji wa tamasha hili utaambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii pamoja na wanamichezo kama vile mpira wa pete, mpira wa miguu, kuvuta Kamba, kukimbiza kuku na michezo mingine.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi