Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa, wale waliohusika na uhalifu wa vishikwambi kwenye maeneo yaliyoripotiwa ya Arusha na Katavi kuviwasilisha vifaa hivyo haraka iwezekanavyo kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa kwa waliohusika.
Hata hivyo, ametoa wito kwa Makarani wa Sensa ambao wanaendelea na zoezi hilo muhimu kwa taifa letu kuwa makini na vifaa hivyo kwani kutokana na uchunguzi imeonekana kuna uzembe unaofanywa na baadhi ya makarani na kuwataka makarani hao kuendelea kuzingatia mafunzo/maelekezo waliyopewa.
Aidha, hadi sasa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaendelea vizuri kwenye maeneo yote nchini.