Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Idara ya Maafa Yawajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maafa
Nov 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22458" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .[/caption]

Na. MWANDISHI WETU

Ofisi ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Warsha hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti ya Maafa"

[caption id="attachment_22459" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.[/caption]

Akifanua mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.

"Warsha hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya kupambana na majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na sababu za kutokea, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia, kupunguza  madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama

[caption id="attachment_22460" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22461" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili kutoa uelewa wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12, 2017. (Picha zote na ofisi ya Waziri Mkuu – Dodoma)[/caption]  

Sambamba na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini kwa kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Pamoja na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka 2004 ambayo inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika shughuli za Manejimenti ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.

Aidha mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza zaidi katika kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi