Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Idara ya Habari-MAELEZO Yapongezwa kwa Utoaji Taarifa kwa Wananchi
Nov 09, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), umeipongeza Idara ya Habari - MAELEZO na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kwa kuimarisha utendaji wake na kuwezesha Wananchi kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jijini Dodoma baada ya Umoja huo kutembelea Ofisi hiyo ambapo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Bw. Deodatus Balile amepongeza jitihada na hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha upatikanaji wa habari kwa wananchi.

“Taasisi nyingi za Serikali zilikuwa hazitoi taarifa zinasubiri kuombwa taarifa, sasa kwa utaratibu huu wa kuzileta taasisi za serikali kuja kutoa taarifa kwa wananchi kupitia Idara hii umezifanya kutoa taarifa bila kusubiri kuombwa", alisisitiza Balile.

Akifafanua, Balile amesema kuwa habari ni haki ya msingi kwa kila mwananchi, inawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati kwa kuzingatia taarifa wanazopata.

“Tunaipongeza Idara kwa kuwa na utaratibu wa kurusha matangazo mubashara kupitia televisheni na televisheni mtandao” ameongeza Balile.

Kwa upande wake, Dkt. Rose Reuben ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji TAMWA na mjumbe wa CoRI amesema wameridhishwa na wanapongeza jitihada zinazofanyika katika kuwawezesha wananchi kupata taarifa sahihi.

“Tunakupongeza Mkurugenzi na Msemaji Mkuu wa Serikali kwa hatua zilizochukuliwa katika kuwezesha wanawake kupata taarifa sahihi na kwa wakati zinazowawezesha katika shughuli zao aidha tunakupongeza uwepo wa watumishi wa kike katika Idara, tunaamini idadi yao itaendelea kuongezeka ili waweze kuendelea kutoa mchango na wao kujifunza zaidi” ameongeza Dkt. Rose.

Wajumbe wa CoRI wametembelea Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO leo Novemba 9, 2022 na kukutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa pamoja na Watumishi wa Idara hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi