Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Idadi ya Watalii Nchini Yazidi Kuongezeka
Mar 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29599" align="aligncenter" width="839"] Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala akihutubia Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_29600" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Meje Jenerali Gaudensi Milanzi akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.

Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143  mwaka 2017 hali iliyopelekea  kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

Akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala amesema Wizara hiyo itaendelea kuvutia watalii zaidi ili kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa.

“Mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 2.1 mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani Bilioni 2.2 mwaka 2017” Alisisitiza Kigwangala

[caption id="attachment_29602" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii wakifuatilia hotuba Waziri wa Mali Asili na Utalii mhe. Dkt. Hamis Kigwangala ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo mjini Dodoma.[/caption]

Akifafanua Dkt. Kigwangala amesema lengo la Serikali ni kuona mafanikio haya yanazidi kuimarika, hivyo kila mtumishi katika Wizara hiyo lazima atimize wajibu wake  ipasavyo.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha majukumu ya Wizara hiyo ipasavyo ni muhimu kuwa na bajeti ambayo itawezesha kushughulikia changamoto za migogoro ya mipaka katika maeneo ya hifadhi, kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali, upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea kazi, kutoa elimu ya maadili na kusimamia watumishi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudensi Milanzi amesema kuwa Wizara hiyo itazingatia ushauri unaotolewa na watumishi wake ili kuongeza tija katika kutatua changamoto zinazojitokeza.

“Wizara itaendelea kupambana dhidi ya ujangili, biashara haramu ya nyara na magogo na kuwachukulia hatua kali watumishi wote watakaogundulika kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kushiriki katika vitendo hivyo “ Alisisitiza Meja Jenerali Milanzi

Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 iliendelea na utaratibu wa kuendeleza watumishi katika mafunzo ya aina mbalimbali kama ifuatavyo:-Jumla ya watumishi

[caption id="attachment_29603" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Meje Jenerali Gaudensi Milanzi pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi.[/caption]

wanne (4) wanahudhuria mafunzo ya muda mrefu nje na ndani. Aidha, mtumishi mmoja(1) yupo nje ya nchi.

Watumishi wengine  kumi na moja (11) walihudhuria mafunzo ya muda mfupi. Mafunzo haya yalihusu watumishi wa kada mbalimbali.

Jumla ya watumishi saba (7) wamehudhuria mafunzo ya ujasiliamali unaohusiana na maandalizi ya kustaafu. Aidha, Wizara bado inaendelea na utaratibu wa kuwaandaa watumishi wote wanaokaribia kustaafu kuhakikisha wanapata mafunzo hayo.

Wizara ya Mali Asili na Utalii imekuwa ikipambana na ujangili, biashara haramu ya nyara, magogo na kuwachukulia hatua kali  za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wote watakaogundulika kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kushiriki katika vitendo hivyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi