Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hivi Ndivyo Chemba Ilivyowasikia, Kuwafikia Wananchi
Nov 01, 2023
Hivi Ndivyo Chemba Ilivyowasikia, Kuwafikia Wananchi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Bi. Siwema Juma akizungumza kuhusu maendeleo yaliyopatikana wilayani humo tangu Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani Machi 19, 2021.
Na Ahmed Sagaff

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Bi. Siwema Juma amewaeleza kuhusu maendeleo yaliyopatikana wilayani humo tangu Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio hayo jijini Dodoma leo, Bi. Siwema amesema halmashuri anayoiongoza imepokea shilingi bilioni 17.3 kutoka Serikali Kuu, kati ya hizo shilingi bilioni 3.6 zikielekezwa kwenye sekta ya elimu.

"Chemba imetekeleza miradi ya elimu ya msingi ndani ya miaka mitatu kwa shilingi bilioni 3.6, hii imehusisha vyumba vya madarasa 68, miundombinu ya maji, nyumba za walimu tatu, matundu ya vyoo 182, shule mpya nne, bweni la wanafunzi wenye uhitaji maalum.

"Kwa upande wa elimu ya sekondari, zimeongezeka shule mbili ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, tumejenga maabara, shule mpya za kata tatu, miundombinu ya maji, nyumba tatu za walimu, na matundu ya vyoo 61," ameeleza Bi. Siwema.

Katika kufikisha huduma ya afya kwa wananchi, shilingi bililioni 4.2 zimetumika kujenga zahanati 11, vituo vya afya viwili, ukamilishaji wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa nyumba ya mtumishi na ununuzi wa vifaa tiba, hivyo, imeifanya Chemba kuwa na jumla ya zahanati 40, vituo vya afya sita na hospitali ya wilaya moja.

"Pia, tumejenga ghala la kuhifadhia mazao kwa gharama za shilingi  bilioni moja, majosho matano kwa shilingi milioni 87, uzio wa mnada kwa shilingi  262 na miundombinu ya usafi kwenye mnada kwa shilingi milioni 25 pamoja na masjala ya ardhi kwa shilingi milioni 62," amedokeza Bi. Siwema.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi