Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hatutamvumilia Atakayehujumu NHIF- Mama Makinda
May 22, 2017

Na Grace Michael, Kigoma

MWENYEKITI wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mama Anne Makinda amesema, kuwa NHIF haItamvumilia yoyote atakayejaribu kuhujumu huduma za mfuko huo kwa manufaa yake binafsi na badala yake atahakikisha unaendelea kunufausha wanachama kwa ujumla. Mama Makinda ameyabainisha hayo hivi karibuni Mkoani Kigoma wakati akizindua mpango wa huduma za Madaktari Bingwa unaotekelezwa kwa wiki nzima katika mikoa ya Kigoma na Geita kwa ushirikiano wa Mfuko na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. [caption id="attachment_1402" align="aligncenter" width="800"] Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambao baadhi yao ni wagonjwa waliofika katika uzinduzi wa huduma za Madaktari Bingwa mjini Kigoma.[/caption] [caption id="attachment_1405" align="aligncenter" width="800"] Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benrard Konga akitoa maelezo ya awali ya zoezi la huduma za Madaktari Bingwa wakati wa uzinduzi wa huduma hizo.[/caption] Aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa wananchi wote kuulinda Mfuko huo wa Bima ya Afya na kujiunga na huduma zake kwa kuwa ni mfumo unaorahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu unaotumika kote duniani. “Hakuna mtu binafsi atakayetumia Mfuko huu kwa maslahi yake binafsi na sisi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hatutakubali kuona mtoa huduma yoyote akiharibu sifa nzuri ama utendaji ambao umeimarishwa kwa kipindi kirefu kwa ajili ya wanachama wetu, tutasimamia huduma zetu kwa nguvu zote,” alisema Mama Makinda. Aidha Mama Makinda ameonya tabia za baadhi ya watumishi wa sekta ya afya ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kunyanyasa wagonjwa na kusema kuwa huduma za afya ni huduma za msingi ambazo hazitakiwi kuchezewa na mtu yoyote ama kutolewa kwa utashi wa mtu binafsi. [caption id="attachment_1408" align="aligncenter" width="800"]  Madaktari Bingwa ambao watashiriki katika zoezi la kutoa huduma katika Hospitali ya Maweni Mkoa wa Kigoma.[/caption] [caption id="attachment_1409" align="aligncenter" width="800"] Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Mama Anne Makinda wakimsaidia Mama mlemavu aliyefika hospitalini hapo kwa lengo la kuhudumiwa na Madaktari Bingwa.[/caption] Akizungumzia utaratibu unaoendeshwa na NHIF wa kupeleka madaktari Bingwa alisema kuwa, Mfuko uliamua kuchukua uamuzi wa kutoa huduma hizi za kibingwa katika Mikoa ambayo ina upungufu wa huduma hizo ili kuhakikisha kila Mtanzania anajivunia uwepo wa Mfuko huo. “Pamoja na huduma hizi Mfuko unazo fursa nyingi hususan za uboreshaji wa huduma za afya kupitia mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo hivyo tumieni hii fursa kujitathmini ili vituo mshirikiane na Mfuko katika uboreshaji wa sekta hii,” alisema Mama Makinda. Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Samson Anga aliishukuru NHIF kwa kutoa kipaumbele cha kupeleka Madaktari bingwa kwa Mkoa wa Kigoma  ambao una mahitaji makubwa ya wataalam hao. “Kwa kweli niushukuru sana Mfuko huu kwa jitihada mnazofanya na kama ambavyo mnaona hali ilivyo wananchi wamefurika hapa kwa ajili ya kupata huduma hivyo zoezi hili litaleta manufaa makubwa ya afya za wananchi wa Kigoma,” alisema Bw. Anga. [caption id="attachment_1410" align="aligncenter" width="800"] Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Makinda akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri huduma za Madaktari Bingwa.[/caption] Akitoa maelezo ya awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema kuwa zoezi hili limefanyika katika Mikoa 16 na sasa linafanyika kwa mara ya 17 na jumla ya wananchi 13,167 walihudumiwa huku wagonjwa 460 wakifanyiwa upasuaji wa magonjwa mbalimbali. Bw. Konga alisema kuwa NHIF inatekeleza maagizo ya Serikali ya kusogeza huduma za kwa wananchi na katika huduma hizi Mfuko umejipanga katika kiwango cha juu kuhakikisha zinanufaisha wanachama na wananchi kwa ujumla. Hata hivyo Bw. Konga ametumia fursa hiyo kuzungumza na wanachama wa Mfuko kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili lakini pia kupata mrejesho wa huduma wanazopata kupitia vituo vilivyosajiliwa na Mfuko. Utaratibu huu amekuwa akiufanya katika hospitali mbalimbali kwa lengo la kutatua changamoto za wanachama na kuboresha huduma za wanachama na kuweka utaratibu mzuri utakaorahisisha wananchi wengi zaidi kujiunga na NHIF.    

Mipangilio
Marekebisho ya Lugha
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi