Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Halmashauri Zaagizwa Kupanda Miti 6000 ya Matunda.
Dec 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Tiganya Vincent, RS TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeziagiza Halmashauri zote kuanza upandaji wa miti ya matunda 6,000 kila moja katika Taasisi na Shule na miti isiyo ya matunda ili kutekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizindua awamu ya pili ya upandaji miti kwa Wilaya ya Igunga ambapo miti 280 ilipandwa.

Mwanri alisema kuwa miti hiyo ni sehemu ya miti milioni na laki tano (1,500,000) kwa kila Halmashauri kila mwaka iliyoagizwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Alisema kuwa kila Halmashauri ni lazima pamoja na kupanda miti ya aina nyingine ianze kupanda matunda katika Shule mbalimbali na Taasisi kama vile Hospitali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi na wagonjwa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kila siku anahitaji apate taarifa na takwimu kuhusu maeneo ambapo miti imepandwa na kiwango chake kwa siku.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wote kusimamia Sheria za Mazingia ili kukabiliana na waharibifu katika mistu mbalimbali ikiwemo wakati ovyo miti.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kurejesha uoto wa asili na viumbe wengine ambao walikwishaanza kutoweka kutokana na uharibifu wa mistu.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza kuhakikisha wanapanga matumizi mazuri ya ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo, huduma za jamii, ufugaji , mistu na uwekezaji.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alisema kuwa hatamuonea huruma mtumishi au mwananchi yoyote atakayekaidi zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo.

Aliongeza kuwa hivi wanaendelea na zoezi kukamata mifugo yote inayozurura mjini na kuharibu miti na wahusika kutozwa adhabu.

Mwaipopo alisisitiza kuwa lengo lao ni kutaka uoto wa asili katika Wilaya ya Igunga unarejea na kuwavutia watu wengi kwenda kuangalia madhari ya kuvutia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga Revocatus Kuuli alisema kuwa hadi hivi wameshatumia kiasi cha milioni 15 katika zoezi la upandaji miti.

Alisema kuwa wataendelea kupanda katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo ili kurejesha mimea ya asili ya eneo hilo.

Hadi jana jumla ya miti 3,233 ilikuwa imepandwa na Halmashauri mbalimbali isipokuwa Urambo ndio ilikuwa haijapanda

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi