Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Halmashauri Zaagizwa Kuanzisha Mifuko ya Dawa
May 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_31067" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Luhota pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kalambo zilizopo Iringa vijijini wakati alipokuwa njiani kuelekea Wilayani Kilolo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.[/caption]

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dar es Salaam

Halmashauri nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za tiba katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwenye maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa leo na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Rais Magufuli amesema kuwa kuanzishwa kwa mifuko hiyo kutasaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa urahisi kwakuwa halmashauri zitakuwa na uwezo wa kununua moja kwa moja kupitia fedha zitakazotokana na mifuko hiyo.

[caption id="attachment_31069" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Luhota pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kalambo zilizopo Iringa vijijini wakati alipokuwa njiani kuelekea Wilayani Kilolo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.[/caption]

“ Natumia fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba (Drug Funds), hili isaidie katika kurahisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo yenu”, alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.

Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba Serikali imetenga Sh50 bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2018/19 kwa lengo la kuboresha huduma ya afya katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Aidha Rais Dkt. Magufuli ametoa rai kwa wakulima nchini kutokubali kulipa tozo ambazo zimeondolewa ikiwa ni pamoja na kulipia ushuru wa mazao kwa mzigo usiozidi tani moja. Nakuongeza kuwa watendaji watakao kaidi agizo hilo na kuendelea kuwalipisha tozo za mazao zilizofutwa ata sita kuwachukulia hatua.

  [caption id="attachment_31070" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi kwa kuimba nyimbo na vijana chipukizi wa Kilolo mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. (Picha na: Ikulu)[/caption]

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jaffo amesema kuwa alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuboresha sekta ya afya nchini ambapo amesema kuwa Serikali tangu ipate uhuru ilikuwa na Hospitali 77 tu lakini kutokana na dhamira hiyo ndani ya kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu Serikali imetenga Sh105 bilioni kwa ajili ya kujenga Hospitali mpya 67 kitendo ambacho kinapelekea kuwa cha kihistoria.

Jaffo aliongeza kuwa sekta hiyo inaendelea kuboreshwa kufuatia kuwepo mpango kabambe wa kujenga vituo vya afya 208 ili kuosogeza huduma za upasuaji karibu na wananchi, na kusema kuwa haya ni mageuzi makubwa ukilinganisha na vituo vya afya 115 kati ya 515 ndivyo vilivyokuwa na hadhi ya upasuaji tangu tupate uhuru.

“Mhe. Rais nitakuwa mnyimi wa fadhira kama nisipokupongeza wewe binafsi na Serikali yako ya Awamu ya Tano, kwa kazi nzuri inayofanyika ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya, mengine sitayasemea nakuachi wewe mwenyewe uyasemee likiwemo la ununuzi wa dawa,” alisema Waziri Jaffo.

Waziri Jaffo alisema kuwa miradi ya ujenzi wa Hospitali kama hiyo inaendelea pia katika wilaya za Siha, Buchosa na Mvomero.

Tayari Serikali imeshatoa shilingi bilioni 4.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mionzi (Radiology), jengo la mama na mtoto(RCH), jengo la maabara na jengo la wodi za kulaza wagonjwa, ambapo intarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi Agosti 2018.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi