Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hakikisheni Wafanyakazi Wanashiriki Michezo-Mhe. Samia Suluhu
Mar 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29502" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma.[/caption]

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Waajiri ambao ni wanachama wa SHIMMUTU wametakiwa kuhakikisha wanahamasisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu kwenye michezo mahala pa kazi ili waweze kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao..

Hayo yameelezwa leo, Mjini Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya SHIMMUTA.

"Ili tuweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ni lazima kwanza tuwe na afya njema. Ikumbukwe kuwa Serikali ilianzisha mashirikisho ya michezo ya wafanyakazi kwa lengo la kuimarisha afya ili waweze kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao," alisema Mhe. Samia.

[caption id="attachment_29509" align="aligncenter" width="900"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus William mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo leo mjini Dodoma.[/caption]

Aidha amesema, ameongea na Balozi wa China na amekubali kusaidia baadhi ya mambo yanayohusu Shirikisho na tayari jitihada za kusaidia ziko katika hatua nzuri.

Hata hivyo amewataka wadau wengine wa michezo kujitokeza na kudhamini mashindano ya SHIMMUTA yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu kwani ni fursa muhimu kwa wadau hao kujitangaza na kutangaza biashara zao na huduma nyingine wanazotoa.

[caption id="attachment_29508" align="aligncenter" width="900"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SHIMUTA mara baada ya kufungua mkutano huo leo mjini Dodoma.[/caption]

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nicholas William akiongea kwa niaba ya Waziri Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Wizara itaendelea kusimamia kwa karibu shughuli za michezo na kuhakikisha wafanyakazi wanashiriki kikamilifu katika michezo mbalimbali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi