Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wakishuhudia jambo kupitia simu ya mkononi ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula (mwenye ushungi mweusi) alipokuwa wakiwaeleza umuhimu wa kutekeleza miradi yenye kuleta matokeo chanya.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro akiwa katika ziara yake ya kwanza baada ya kukagua shughuli mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara yake. Kulia ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao na Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Emmanuel Mhando.
Wakuu wa Idara Mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula alipotembelea Wilaya ya Ngorongoro kukagua miradi inayosimamiwa na Wizara anayoiongoza.