[caption id="attachment_38520" align="aligncenter" width="750"] RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman kuhudhuria hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W ).[/caption]
NA Abdi Shamnah, Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, jana amejumuika na mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu kutoka mikoa yote ya Unguja kuadhimisha uzawa wa Mtume Muhammad (SAW).
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Maisara mjini hapa, ambapo Viongozi mbali mbali wa dini na serikali, mabalozi na wanafunzi kutoka madrasa na vyuo vya Qur'an waemeshiriki.
Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW), huadhimishwa kila ifikapo mwezi 11, Rabi - Ul -Awal ya kila mwaka.
Akitoa waadhi kwa waislamu waliohudhuria Maulid hayo, Mstahiwa Naibu Kadhi Mkuu, Khamis Othman Kombo alitoa wito kwa waumini wa dini hiyo kuendeleza wajibu wa kufuata maadili na mwenendo mwema aliokuja nao Mtume, akibainisha kuwa hatua hiyo ni ukamilifu wa imani.
Alisema kuja kwa utandawazi Duniani, kumeifanya jamii ya Wazanzibari na hususan vijana kujiingiza katika mambo maovu, ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia na hivyo kwenda kinyume na miongozo wa dini.
Aliwakumbusha waislamu wajibu wa kutekeleza kwa dhati yale yote aliyokuja nayo Mtume kwa kuwa yeye ndio kigezo chema kutoka kwa Mola muumba.
Aidha, aliishukuru Serikali kwa kudumisha amani n utulivu nchini muda wote, hali inayotoa nafasi kwa wananchi kupata fursa adhimu ya kuabudu.
Nae, Sheikh Mohammed Kassim kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, alikemea tabia iliojengeka miongoni mwa waumini ya kushindwa kufuata maadili na tabia njema alizokuwanazo Mtume Muhammad (SAW).
“Inatupasa kubadili nyendo na tabia zetu na kufuata maadili na mwenendo mwema aliokuwa nao mtume wetu”, alisema.
Alisema jamii ya kizazi kiliopo imeyapa kisogo mafunzo aliyokuja nayo Mtume kwa kushindwa kuwaheshimu na kuwatii wazee, hivyo kwenda kinyume na mwenendo aliodumu nao ikiwa ni kigezo cha unyenyekevu.
Alibainisha kuwa Mtume Muhammad (SAW) amesifiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa na tabia nzuri, hivyo aliwataka waumini kufuata mwenendo wake pamoja na kushinda changamoto mbali mbali zinazotokana na utandawazi.
Aidha, Sheikh Kassim aliwataka waislamu kujikita katika utamaduni wa kumsalia Mtume pale anapotajwa, kuvuta tasbikh pamoja na kufanya istifar ili kupata fadhila, huku akiwaonya baadhi ya waumini (walioibuka katika siku za hivi karibuni) wanaopinga ibada hizo.
Maadhimisho ya Maulid ya uzawa wa Mtume Muhammad (SAW), yalifunguliwa kwa Qoraan tukufu, iliyosomwa na Ustadhi Mtumwa Juma Kombo kutoka Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja .
Aidha, yaliambatana na usomaji wa Milango sita (6) ya Barazanji, Maulid ya Homu kutoka Mtendeni mjini Unguja pamoja na usomaji wa Kaswida kutoka Madrsa mbali mbali.
[caption id="attachment_38521" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, pamoja na viongozi wa dini na serikali wakisikiliza Qaswida ya Kumtakia Rehema Mtume (S.AW) kabla ya kuanza kwa hafla ya Maulid iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.[/caption] [caption id="attachment_38523" align="aligncenter" width="750"] Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na wake wa viongozi mbalimbali na wananchi waliohudhuria Maulid Matukufu ya kuazaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.[/caption] [caption id="attachment_38524" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar waliohudhria hafla ya Maulid Matukufu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya mpira vya Maisara Suleiman Unguja, Zanzibar.[/caption] [caption id="attachment_38532" align="aligncenter" width="750"] Sheikh Mohammed Kassim, kutoka Ofisi ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar, akisoma Khutba ya Kiswahili, wakati wa sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar.[/caption] [caption id="attachment_38531" align="aligncenter" width="750"] Wanafunzi wa Madrassa Qadiriya, kutoka Amani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakiwa katika Qiyamm wakimsalima Mtume Muhammad (S.A.W) skwenye sherehe za mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar.[/caption] [caption id="attachment_38522" align="aligncenter" width="750"] Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh. Hassan Othman Ngwali, akizungumza na kutoa maelezo ya hafla hiyo ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar.[/caption] [caption id="attachment_38527" align="aligncenter" width="683"] Ustadh Mohammed Haji Khatib, kutoka Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja, akisoma mlango wa kwanza Barzanj katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.(Picha na Ikulu)[/caption]