Dkt. Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Hospitali ya Wete na Skuli ya Msingi Kojani Pemba
Jul 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Wete Pemba inayojengwa katika Kijiji cha Kinyasini, kupitia Fedha za Uviko -19, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya na (kulia ) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis, akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo 25-7-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akiwasalimia Wananchi wa Kojani alipowasili kwa ajili ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Kojani inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk na Mkuuwa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Kojani Pemba baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Kojani, inayojengwa kwa Fedha za Uviko -19,leo 25-7-2022, akiwa Pemba akiendelea na ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa miwili ya Pemba