Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Mwinyi Awaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni
Nov 15, 2024
Dkt. Mwinyi Awaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Iddi Said Khamis kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.
Na Ikulu - Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wawili aliowateua hivi karibuni.

Viongozi walioapishwa ni Mhe. Iddi Said Khamis, Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Mwinyi tarehe 24, Oktoba 2024. 

Kabla ya uteuzi huo, Kadhi Iddi Khamis alikuwa Mrajis wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg. Hiji Dadi Shajak,kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.

Mwengine ni Ndg. Hiji Dadi Shajak, Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. 

Kabla ya wadhifa huo, Ndg. Shajak alikua Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kurusha Maudhui, Zanzibar (ZMUX). Aidha, Shajak aliteuliwa Septemba, 25 mwaka 2024 kushika majukumu mapya.

Wakizungumza kwenye hafla ya uapisho huo, iliyofanyika Ikulu, Zanzibar, viongozi hao walimuahidi Rais Dkt. Mwinyi kuyafanyia kazi maelekezo yake yote na kuendeleza jitihada ya taasisi mpya wanazozitumikia kwa kuendeleza ushirikiano kwa Serikali na wadau wengine.

Hafla ya uapisho huo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, viongozi wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na Masheikh kutoka Ofisi ya Mufti, Zanzibar.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi