Dkt. Mwinyi Amuapisha Mkurugenzi Mkuu Mpya wa ZAECA
Sep 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi Hati ya kiapo, Ali Abdalla Ali mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akimkabidhi Vitabu Ali Abdalla Ali, ikiwa ni muongozo katika utekelezaji wa kazi zake mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. haroun Ali Suleiman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali (kushoto) wakiwa katika hafla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa ZAECA, Bw. Ali Abdalla Ali (hayupo pichani) leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abduulla (kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, Bw, Ali Abdalla Ali katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akizungumza na Viongozi mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria katika hafla ya kumuapisha, Ali Abdalla Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar pamoja na kutoa maelekezo maalum kwa Mkurugenzi huyo