Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Marry Nagu: Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja mkombozi kwa mkulima
Feb 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="900"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dkt. Mary Nagu wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Kamati hiyo kwa kipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018.[/caption]   Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja(Fertilizer Bulk Procurement) umesaidia kuwawezesha wakulima wadogo kupata mbolea yenye ubora na kwa bei nafuu kwa wakati. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dkt. Mary Nagu wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Kamati hiyo kwa kipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018. Dkt. Nagu amesema kuwa Sera ya Kilimo ya mwaka 2013 inaeleza umuhimu wa kuongeza matumizi ya pembejeo za kisasa kama mbolea, madawa ya kilimo, mbegu bora na zana za kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji mazao, kupunguza umaskini na kuwa na usalama wa chakula na lishe. “Aidha, Kamati ilieleza kuridhika na faida zinazotarajiwa kupatikana kutokana na mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja ikiwamo udhibiti wa bei ya mbolea kwenye soko holela” amefafanua Dkt. Nagu. Aidha, Dkt. Nagu ametaja faida nyingine ya mfumo huo ikiwemo nchi kunufaika kwa ununuzi wa pamoja kwa lengo la kupata punguzo kutokana na kiasi kingi kinachonunuliwa na kupunguza gharama za uendeshaji. “Pia mfumo utaongeza ufanisi kwa kudhibiti mbolea kutoka nje kwa kuagiza mara chache kwa kiwango kikubwa, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo mbolea imekuwa ikiingizwa mara nyingi kwa kiwango kidogokidogo pamoja na kuongeza na kuhamasisha matumizi ya mbolea nchini”ameongeza Dkt. Nagu. Mbali na hayo Dkt. Nagu amesema kuwa kamati imepokea taarifa ya Hali ya Chakula nchini ambapo kwa  msimu wa mwaka 2016/2017 hali ya chakula imeendelea kuimarika kulingana na mavuno mazuri nay a ziada yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi