Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Magufuli Azindua Rada Mbili za Usafiri wa Anga.
Sep 16, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46909" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine kwenye picha ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari pamoja na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier.[/caption]

Na Dianarose  Shirima-MAELEZO.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua RADA za usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICA) na uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) ikiwa ni mwendelezo wa mradi uliokuwa umeanzishwa na serikali ya awamu ya tano kufuatia kuhamasisha safari za ndege na kuendeleza shirika la ndege la Tanzania(ATCL) uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

 Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewapongeza wakandarasi toka Ufaransa waliopewa mradi huo na kuukamilisha mapema kama alivyohimisa hapo awali.

[caption id="attachment_46910" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam[/caption] [caption id="attachment_46911" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Hamza Johari kuhusu utendaji kazi wa Rada hiyo mpya ya kuongozea ndege.[/caption]

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic  Clavier, amesema Ufaransa inaunga mkono katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia viwanda na kusema kuwa Ufaransa ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta maendeleo na kufikia uchumi wa kati kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania. Balozi pia akampongeza Rais Dkt. Magufuli pamoja na watanzania kwa jinsi walivyoungana kwa pamoja ili kuleta maendeleo nchini kwa kasi.

Katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewakaribisha nchi za Afrika na Ulaya kupitisha ndege zao katika anga la Tanzania kwa kuwathibitishia usalama katika anga la Tanzania na kuwataka wasiogope wao wapite katika anga la Tanzania na wataongozwa vizuri, Rais Magufuli amesema kuwa licha ya kuanzisha safari Mumbai, India serikali imelenga kuanzisha na nchi zingine pia duniani, ikiwemo China na London na kusisitiza kuwa zingine zitafuata.

[caption id="attachment_46912" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier mara baada ya kuzindua mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere[/caption] [caption id="attachment_46913" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya vitendea kazi katika kituo cha Mfumo wa Rada cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46914" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere[/caption]   [caption id="attachment_46916" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii Hamonize ambaye alitumbuiza kabla ya uzinduzi wa mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere[/caption] [caption id="attachment_46917" align="aligncenter" width="750"] Muonekano wa Kituo cha Mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Picha namba 8-10. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kukagua eneo la Machinjio ya Ng’ombe na Mbuzi Vingunguti jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua ujenzi wa machinjio ya kisasa ambao unasuasua. (PICHA NA IKULU)[/caption]

Aidha, Rais Magufuli amewataka watanzania kutokukata tamaa pale zinapotokea changamoto katika harakati za kuleta maendeleo,  akasema kuwa hata ndege  iliyokamatwa huko Afrika Kusini ni moja ya changamoto katika maendeleo, hivyo watanzania wanatakiwa kuwa na umoja hata pale changamoto zinapotokea bila kuangalia tofauti zao za kisiasa kwani maendeleo ya Tanzania hayana chama bali yatafaidisha kila mmoja hata wajukuu wa kizazi kilichopo sasa.

Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, kutokana na uchapakazi mahiri aliouonesha katika nafasi hiyo, pia akasema kwa mwaka wa fedha uliopita, Mamlaka hiyo ilikusanya mapato ya Billioni 71 kutoka Billion 40  na kwamba mwaka ujao wa fedha wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Billioni 82.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi