Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Kibona: Tanzania ya Viwanda itaokoa Kilimo hapa Nchini
Oct 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_19342" align="aligncenter" width="750"] Mtaalam wa Kilimo cha Kisasa na Tabibu wa Dawa za Asili Dkt. Samson Kibano akizungumza na Waandsishi wa Habari kuhusu mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo wilaya ya Momba mkoani Songwe katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa aliyeko katika mafunzo kwa vitendo toka Idara ya Habari (MAELEZO[/caption]

Na: Thobias Robert.

Katika kutimiza ndoto ya Tanzania ya uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji viwandani, wadau mbalimbali wa maendeleo wamezidi kujitokeza na kutoa mawazo yatakayosaidia kukuza sekta za kiuchumi ili kutimiza ndoto hiyo  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza katika Dkt. Samson Kibona, kutoka Antipa Herbal Clinic amesema kuwa uchumi wa viwanda utaokoa kilimo cha Tanzania na kupandishwa thamani ya mazao yalimwayo hapa nchini na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.

[caption id="attachment_19345" align="aligncenter" width="750"] Mtaalam wa Kilimo cha Kisasa na Tabibu wa Dawa za Asili Dkt. Samson Kibano akizungumza na Waandsishi wa Habari kuhusu mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo wilaya ya Momba mkoani Songwe katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa aliyeko katika mafunzo kwa vitendo toka Idara ya Habari (MAELEZO) Thobias Robert. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa lengo la kuelezea mbinu za kilimo cha kisasa, kutoa ombi kwa serikali juu ya kusimamia kilimo hicho chenye tija na kitakachopunguza uagizwaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo kutoka nje ya nchi.

“Tanzania ya viwanda itaokoa sekta ya kilimo, kupandisha thamani ya mazao na kufanya mazao yanayolimwa nchini kutosafirishwa nje badala yake bidhaa zitokanazo na mazao hayo kama vile mafuta ya kupikia, vyakula vya kawaida, kama biskuti, nafaka halisi ya unga ndizo zitasafirishwa au kuuzwa nje na kuongeza fedha za kigeni,” alieleza Dkt. Kibona.

Aidha Dkt. Kibona ambaye pia ni mkulima wa kati wilayani Momba alisema kuwa, serikali haina budi kutumia mfumo wa kilimo cha umwagiliaji (Canal System) kama ambavyo mataifa ya Israel, Pakstani na India yamekuwa yanatumia njia hiyo, lakini pia kuondoa utegemezi wa kilimo cha mvua pekee yake ambacho kimekuwa kikitumiwa kutoka karne hadi karne hapa nchi ambacho kimekuwa kikiligharimu taifa pindi hali ya hewa inapobadilika.

Vilevile serikali haina budi kutumia mbegu za kisasa zinazozalisha mazao ya kutosha na yenye tija kwa taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja kuliko kuendelea kutumia mbegu za zamani ambazo zimekuwa zinaathiriwa na kushambuliwa na maradhi pamoja na wadudu.

Aliendelea kusema kuwa kwa taifa la Uingereza lina asilimia 20 ya watu wanaojihusisha na kilimo linatumia mbinu ya Green house ambayo ni njia ya kuchimba shimo na kutumia mitambo ya kumwagilia shamba (Pivot injection system) lakini nchi ya Tanzania ina wakulima wanaofikia zaidi ya asilimia 75 lakini bado wanatumia njia za asili katika uzalishaji wao.

“Tanzania imekuwa ikipokea bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi kama vile mitumba, viatu pamoja na bidhaa zingine, ifike hatua tuanze kutoa bidhaa Tanzania tupeleke nje ya nchi ili turudi na dola mikononi ili tuijenge nchi yetu kwa kutumia pesa zao na siyo wao pekee kutuletea bidhaa zao hapa nchini,” aliezea Dkt. Kibona.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa soko la mazao ya mboga mboga zinazozalishwa hapa nchini ambalo limekuwa na soko kubwa nje ya nchi, serikali haina budi kuhakikisha kuwa inaongeza msukumo na utoaji wa mbolea kwa wakulima ili kurahisisha uzalishaji wa mbogamboga hizo. Vilevile mazao ya mahindi, maharage, soya yanapaswa yageuzwe kuwa mazao ya biashara yanaoyotegemewa kwa pato la taifa kuleta pesa za kigeni kwani mazao hayo yanaishia hapa nchini pekee.

Dkt. Kibona alimuomba Rais Dkt. John Magufuli ahakikishe kuwa kuna upatikanaji wa kutosha wa huduma za ulinzi, umeme, benki, afya pamoja na maji hususani maeneo ya vijijini ili wakulima waweze kuzalisha mazao ya biashara yenye tija kwa ajili ya ushindani wa kimataifa.

“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, iwe inatoa motisha kwa wakulima kama vile kuwapa tuzo wakulima wanaozalisha na kuuza mazao mengi ya biashara na kulipatia taifa fedha za kigeni, kutoa punguzo la bei za pembejeo kwa wakulima hasa vijijini, pamoja na kusimamia vyema bei za mazao ya kilimo hapa nchini na nje ya nchi kwa wakulima wetu,” alifafanua.

Dkt. Kibona ni mtaalamu wa masuala ya kilimo ambaye pia anamiliki kampuni yake inayojihusisha na kilimo wilayani Momba mkoani Songwe  ambaye amekuwa akitumia kilimo chake kama shamba darasa kwa Wananchi na viongozi wa wilaya na Mikoa ya jirani. Vilevile kwa sasa ana mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata mpunga katika eneo la kijiji cha Luasho.

         

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi