Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Jingu Atembelea Gereza Kuu Wanawake Kingolwira
Sep 01, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu ametembelea Gereza Kuu la Wanawake la Mkono wa Mara, Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa ustawi wa wanawake, watoto na wazee wanaotumikia adhabu ya kifungo katika magereza mbalimbali nchini.

DKt. Jingu amesema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuwawezesha wataalam hao kutafuta ufumbuzi wa changamoto za jamii wakiwa na uelewa mpana kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hasa makundi hayo maalum.

Aidha, amesema kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inajumuisha masuala yote yanayohusu wanawake, wazee na watoto kwa hiyo ni muhimu kutafuta suluhisho la matatizo kwa watanzania wote bila ubaguzi na hivyo kuamua kufanya ziara katika magereza mbalimbali kuwasalimia na kuwasikiliza wafungwa.

“Sisi tunashughulikia masuala yote ya Maendeleo ya Jamii wakiwemo hawa waliopo magerezani tukiwatembelea na kuwasikiliza tutakuwa katika nafasi nzuri ya kutafuta suluhisho la matatizo ya kijamii”. alisema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Flora Mbalawa ameipongeza Wizara kwa hatua ya kufanya ziara na kusikiliza maoni na mapendekezo ya watumishi na wafungwa ili kutafuta namna bora ya kutatua changamoto za jamii. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi