Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Abbasi: Tutaionesha Dunia Utamaduni Wetu Kutokea Moshi
Jan 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, leo Alhamisi Januari 20, 2022, amekagua maandalizi ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro.


Katika Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Januari 22, 2022, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Chifu, akitumia jina la Chifu Hangaya. 


“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.


“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni  wetu kuendelea hapa nchini", alisema Dkt. Abbasi. 


Tunataka kutumia utamaduni na sanaa kuileta dunia na kuionesha dunia kile Tanzania ilichonacho,” amesema Dkt. Abbasi kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.


Tamasha hilo limeandaliwa na machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Chifu Frank Marealle na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi