Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Abbasi Atembelea Magazeti ya China, Atoa Wito Kuhusu Habari za Afrika
Oct 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37360" align="aligncenter" width="1008"] Vikao mbalimbali vya majadiliano vikiendelea nchini China kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake pamoja na Maafisa wa nchini humo.[/caption]

Na Beatrice Lyimo- CHINA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano Oktoba 24, 2018  ametembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China  kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

Akiwa katika vyombo hivyo,  Dkt. Abbasi amesema kuwa China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu kwenye masuala mbalimbali hivyo ni muda sasa wa kufanyia kazi mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye masuala ya utamaduni na habari uliosainiwa mwaka 2016

[caption id="attachment_37364" align="aligncenter" width="894"] Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua jambo katika vikao vinavyoendelea Beijing, China.[/caption]

"Lengo la ziara yetu ni kujifunza wenzetu mnavyofanya kazi na pia kutafuta namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya habari," ameongeza Dkt. Abbasi akiwa People's Daily.

Amelitaka gazeti hilo linalomilikiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na linalofikisha habari zake kwa  wasomaji milioni 700 duniani kupitia mitandao mbalimbali kuenzi ushirikiano huo wa muda mrefu kwa kuzipa nafasi pia habari za maendeleo za Afrika na Tanzania.

[caption id="attachment_37363" align="aligncenter" width="1008"] Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake Beijing, China inaendelea ambapo ametembelea Vyombo vya Habari vya People's Daily na China Daily.[/caption]

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete amewakumbusha viongozi wa chombo hicho kuzipa fursa habari za utalii hasa vivutio vingi vilivyoko Tanzania.

Akiwa katika gazeti la China Daily lililoanzishwa na Serikali ya China zaidi ya miongo mitatu iliyopita, Dkt. Abbasi aliwaeleza wahariri wanaohusika na toleo maalum la Afrika kuzingatia kuwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zina maendeleo na vivutio vya uwekezaji  vinavyopaswa kujulikana kwa wekezaji wengi wa China maombi ambayo wahariri wa gazeti hilo waliyakubali.

Dkt. Abbasi anaendelea na ziara yake ambapo atatembelea television za China za CCTV na CGTN na baadaye kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Redio China.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi