Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DC Ruangwa Awataka Wachimbaji Namungo Kuzingatia Sheria
Mar 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41551" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (kushoto), akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (wa pili kushoto), kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa Mkuu wa Wilaya na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga.[/caption]

Na Sylvester Omary - GCLA

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali wanapokuwa wanatekeleza shughuli za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya zao na mazingira.

Mgandilwa ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa wachimbaji hao yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika kwenye kijiji cha Namungo wilayani Ruangwa.

“Nawaomba wachimbaji wa mgodi huu mtumie fursa hii ya mafunzo kujifunza Sheria zinazohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali ili muweze kuzingatia matumizi salama ya kemikali katika shughuli zenu kwa lengo la kulinda afya zenu na mazingira yanayowazunguka kwani natambua uchimbaji wa dhahabu unahusisha matumizi ya kemikali na hakuna kemikali isiyo na madhara duniani, hivyo mafunzo haya yawasaidie kujua namna bora ya kujilinda na madhara bila kuathiri shughuli zenu za uchimbaji”, alisema Mgandilwa.

[caption id="attachment_41552" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Namungo, Mhe. Hashim Mgandilwa (kushoto), akiongea na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wachimbaji hao yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika katika kijiji cha Namungo kilichopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi leo.[/caption]

Alifafanua kuwa sekta ya madini ni sekta muhimu sana katika uchumi na ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuwawekea mazingira mazuri wachimbaji ili kuhakikisha wanafaidikia na kazi hizo pia wanalinda afya zao  kwa kuwa athari za kemikali nyingine zinaweza kuonekana baada ya miaka mingi.

Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo aliwataka wachimbaji hao kujisajili Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kutambulika kama wadau wanaotumia kemikali katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

“Pia, niwaombe wachimbaji wa mgodi huu kutumia mafunzo haya kujifunza namna na taratibu sahihi za kujisajili, hivyo mnapaswa kuuliza maswali pale mnapoona mnahitaji ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa wawezeshaji wa mafunzo kwa lengo la kuboresha shughuli zenu na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawajaweza kupata elimu hii kwa sasa,” Aliongeza.

[caption id="attachment_41550" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (aliyesimama), akiwaeleza washiriki wa mafunzo namna ya utunzaji na matumizi salama ya kemikali kwa wachimbaji wa madini.[/caption] [caption id="attachment_41555" align="aligncenter" width="750"]  Washiriki wa mafunzo ya namna ya utunzaji na matumizi salama ya kemikali kwa wachimbaji wa madini wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (hayupo pichani).[/caption]

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,   Bw. David Elias alisema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuwafikia wadau wake na kuwapa elimu ya matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya kemikali ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya na kimazingira yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali. Vile vile alisisitiza kuwa wachimbaji hao ni sehemu ya wadau wengi ambao Mamlaka imejipanga kuwafikia na kuwapatia elimu hiyo.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji ya Gemini, Alfred Michael ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuamua kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimarisha shughuli zao za uchimbaji hasa kwenye matumizi ya kemikali.

[caption id="attachment_41553" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wawezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Namungo, Bw. Abraham Pasati (wa pili kulia, waliokaa), na washiriki wa mafunzo kutoka mgodi wa Namungo.[/caption]

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuona umuhimu wa kuja kutoa mafunzo haya kwetu kwa sababu yatatusaidia katika kujilinda dhidi ya madhara ya kemikali kwenye kazi zetu za uchimbaji, tunaamini mafunzo haya yatakuwa chachu ya kufuata Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa lengo la kuboresha uchimbaji na kulinda afya na mazingira kwa ujumla”, alisema Michael.

Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya wachimbaji wadogo wadogo 50 kutoka Kampuni za uchimbaji za Gemini na Majini zinazojihusisha na uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Namungo uliopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi