[caption id="attachment_4591" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mapema jana.[/caption]
Na: Frank Mvungi
Serikali imesema imeridhishwa na Utendaji kazi wa Mamalaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kuzingatia Sheria na Kanuni hali inayoongeza tija katika mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema moja ya miradi hiyo ni ule wa kupanua na kusambaza maji katika mji wa Chalinze utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki mbili.
“Kwa ujumla naridhishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika kutekeleza miradi ya maji nawatia moyo muendelee kufanya kazi hii kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie” Alisisitiza Prof. Mkumbo.
[caption id="attachment_4594" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo na kushoto ni Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa.[/caption] [caption id="attachment_4595" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua miundo mbinu ya chanzo cha maji ruvu juu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.(Picha na: Frank Mvungi)[/caption]Akifafanua Prof. Mkumbo amesema katika ziara yake amejionea na kukagua miundo mbinu ya kusambaza maji,ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji na miundo mbinu yote katika chanzo cha maji Wami kinachopanuliwa ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Chalinze .
“Wananchi wajenge utamaduni wa kutunza rasilimali zilizopo ikiwemo miundo mbinu ya maji mbayo inajengwa kwa gharama kubwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi wote na kuchochea maendeleo” Alisisitiza Prof. Mkumbo
Mradi mwingine uliotembelewa ni ule wa uchimbaji visima vyenye urefu wa mita 600 kila kimoja vipatavyo 20 na kati ya hivyo 17 vimekamilika hivyo kuongeza upatikanaji wa maji ambao utachochea maendeleo na ukuaji wa sekta ya Viwanda.
[caption id="attachment_4596" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. E. Mukasa (katikati)akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo.[/caption] [caption id="attachment_4600" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya mitambo katika chanzo cha maji ruvu juu,kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo.[/caption]Visima hivyo vitawezesha kuzalishwa kwa lita milioni 260 za maji kwa siku zitakazotumika katika Wilaya ya Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Romanus Mwangi’ngo amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini na Visima vya Kimbiji na Mpera vitasaidia kufikisha kiwango cha maji yanayozalishwa kufikia lita milioni 756 zitakazosaidia katika kuondoa tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam.
[caption id="attachment_4601" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya miundombinu ya katika chanzo cha maji Ruvu juu.[/caption]Aliongeza kuwa kwa upande wa mradi wa Chalinze vituo vya kusambaza maji takribani 236 vimeshajengwa kati ya 351 vilivyopangwa hali inayoonyesha kuwa mradi huo unaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa na utakamilika mwezi oktoba 2017.
Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotelezwa na DAWASA katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu,Mradi wa uchimbaji Visima virefu Kimbiji na Mpera,Chanzo cha maji Wami unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.