Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DAWASA Waaswa Kuendelea Kuwa Wazalendo Katika Kutekeleza Miradi ya Maji.
Mar 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisalimiana na Watumishi wa Mamlaka  ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakati wa ziara yake katika mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akifurahia jambo wakati akizungumza wa Watumishi wa Mamlaka  ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakati wa ziara yake katika mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Mamlaka  ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakufuatilia hotuba ya  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ziara yake katika Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) kuendelea kuwa wazalendo na kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa  ili kuongeza kasi ya maendeleo wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika mamlaka hiyo Mhandisi Kamwelwe amewataka Wafanyakazi  hao kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kutekeleza majukumu yao ambayo ni kuboresha huduma za maji safi na majitaka katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na Mji  wa Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

" Vifaa vya ujenzi wa miradi  ya maji hususan mabomba vinunuliwe katika viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuimarisha uchumi wa viwanda, " alisisitiza Kamwelwe.

Kamwelwe amesema, kwa kutumia vifaa vinavyozalishwa hapa nchini viwanda husika vitanufaika na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya DAWASA Bw. Laston Msongole alieleza  mipango mbalimbali ya kimapinduzi ambayo inatekelezwa na Mamlaka hiyo ili kuwezesha miradi kutekelezwa kwa wakati,  kwa ubora na kwa kuzingatia mahitaji na hali halisi ya Taifa.

Awali Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Romanus Mwang'ingo alitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ambapo alitaja miradi kadhaa ya kimkakati kuwa imekamilika na baadhi ikiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.

Ameitaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na  upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini, ujenzi wa bomba kuu la mita 1.8 kutoka  katika mtambo huo hadi jijini Dar es Salaam, upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu, ujenzi wa mabomba makuu kutoka katika mtambo huo yenye vipenyo vya mm 1200, 1000 na 900 pamoja na  ujenzi ta tenki la kibamba lenye uwezo wa mita za ujazo  10,000,000.

Aliongeza kuwa mradi ya uboreshaji wa mfumo wa usambazaji inayojumuisha matenki 9,  vituo vya kusukuma maji  na ulazaji wa mabomba kwa taribani kilometa zaidi ya 400, upo katika hatua za mwisho kukamilika.

DAWASA imekuwa chachu ya kutatua changamoto ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwa kutekeleza miradi  ya kimkakati  hali inayochochea upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi