Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DAWASA kuwaunganisha wananchi 40,000 na huduma ya maji
Sep 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36016" align="aligncenter" width="744"] Mafundi wakiendelea na kazi ya uchimbaji mtaro tayari kwa kulazwa mabomba ili kuwaunganisha wateja elfu 40,000 katika eneo la Salasala Jijini Dar es Salaaam.[/caption] [caption id="attachment_36014" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya mabomba yanayotumika katika mradi huo wa kuwaunganisha wateja elfu 40,000 na huduma ya maji.[/caption] Na; Mwandishi wetu

 Jumla ya wateja wapya 40,000 wanatarajiwa kuunghanishiwa huduma  ya maji katika eneo la Salasala Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua za Serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka hiyo, Dhamira yake ni kuhakikisha kuwa  kazi hiyo inafanywa kwa weledi  na kuzingatia maslahi ya wananchi na ustawi wa Jamii.

Awamu ya kwanza itaanza kwa kuwaunganisha wananchi wanaoishi eneo la Sasasala Jijini Dar es Salaam kwani eneo hilo tayari lina mtandao na maji kutoka mtambo wa ruvu chini.

Aidha, katika mikoa mingine DAWASA inatekeleza  miradi midogo ya kusogeza huduma kwa wateja inayoendelea ambapo miradi hii yote inagharimiwa na DAWASA na wateja wataunganishiwa maji kwa mkopo.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) imeunda kikosi maalum cha kufanya kazi  ili kuongeza wateja na kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge.

Katika kuhakikisha kuwa kazi ya kuwaunganishia maji wananchi wa eneo la Salasala, mradi huo utasimamiwa na  wahandisi 3 , mafundi 3 na Vijana kutoka chuo cha VETA.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbli inayolenga kuhakikisha kuwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na Pwani wanapata huduma bora ya maji na hivyo kuchochea maendeleo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi