[caption id="attachment_29607" align="aligncenter" width="886"] Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Assad akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kauli yake aliyoitoa wakati akiwasilisha ripoti za Ukaguzi wa fedha kwa mwaka unaoishia June 30, 2017 kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Kulia ni Naibu mkaguzi mkuu wa hesabu za Taifa Bw. Athumani Mbuttuka na kushoto ni Naibu mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali anayeshughulia Mamlaka za Serikali za Mitaa Bw. Jasper Mero.[/caption] [caption id="attachment_29609" align="aligncenter" width="895"] Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Assad uliofanyika leo mjini Dodoma.[/caption]
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.
Serikali imesema kuwa Deni la Taifa ni stahimilivu hali inayoonyesha kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Taifa letu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Juma Assad amesema kuwa hadi kufikia tarehe 30 June 2017 deni la taifa lilikuwa trilioni 46.08 ambapo deni la ndani ni shilingi trilioni 13.34 sawa na asilimia 29.
Akifafanua amesema kuwa matokeo ya ukaguzi huo yatawekwa wazi mara baada ya ripoti husika kuwasilishwa rasmi Bungeni kabla ya tarehe 12, April 2018 na baada ya hapo nakala ngumu za vitabu zitapatikana kwenye Ofisi zote za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na kwenye tovuti (www.nao.go.tz).
Kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005), mnamo machi 27, 2018 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad aliwasilisha ripoti ya ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha unaoishia June 2017 kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.