Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bunge la Tanzania na Morocco Wakubaliana Kuimarisha Ushirikiano
Sep 18, 2023
Bunge la Tanzania na Morocco Wakubaliana Kuimarisha Ushirikiano
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto), akiwa ameambatana na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco, Mhe. Rachid Talbi El Alami akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake katika nchi hiyo katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.
Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco, Mhe.  Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mabunge ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara. 

 

Aidha, Dkt. Tulia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Serikali ya Morocco kwa vifo vya watu zaidi ya 3,000 vilivyosababishwa na madhara na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mapema mwezi huu.

Pia, amepongeza juhudi zilinazofanywa na nchi hiyo katika kukabiliana na maafa pamoja na changamoto zilizotokana na tetemeko hilo. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi