Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bonanza la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Dodoma lafana
Jul 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33804" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka na akishiriki mazoezi ya mbio za polepole(jogging) na viongozi wengine wa Serikali wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma. Bonanza hilo limeandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na limefanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma[/caption]

Na. Georgina Misama – MAELEZO

Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo yapongezwa kwa kuandaa Bonanza lilihudhuriwa na mamia ya Watumishi kutoka Wizara zote pamoja na baadhi ya Taasisi.

Lengo la Bonanza hilo ni kuwakaribisha Dodoma watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za umma waliohamishiwa kutoka Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi katika Boanza hilo alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi ambaye aliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.  Florens Turuka.  

[caption id="attachment_33805" align="aligncenter" width="800"] Viongozi mbalimbali wa Serikali wakishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa mbio za polepole(jogging) wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri.[/caption] [caption id="attachment_33806" align="aligncenter" width="800"] Kikundi cha Jogging kutoka Dodoma kikishiriki katika Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri.[/caption]

Akizungumza katika hotuba yake fupi, Dkt. Turuka aliipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo kwa kuandaa bonanza hilo lililopata mwitikio mkubwa kutoka kwa watumishi wa Mawizara yote.

“Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza sana wananchi washiriki katika michezo na mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya na kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa” alisema Prof. Turuka.

Turuka alisema kwamba  mpango wa Serikali kuhamia Dodoma lilikuwa wazo la muda mrefu na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza mpango huo, na kuwahamasisha watumishi hao kufanya michezo iwe endelevu kwani ni jambo linaloboresha uhusiano mzuri kati ya mtumishi mmoja na mwingine ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya ya mwili na akili sambamba na kuboresha utendaji wa kazi.

[caption id="attachment_33807" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka,Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi Sihaba Nkinga wakishiriki katika Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri.[/caption] [caption id="attachment_33808" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi wakikagua timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri.[/caption]

“Kama ambavyo kuna sheria na taratibu katika kila mchezo tulioshiriki hapa leo, tujifunze pia kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu kazi ”. alisema Dkt. Turuka.

Aidha, Dkt. Turuka aliwapongeza viongozi wote waliohudhuria Bonanza hilo kwa kuongoza kwa mafano, kwani  viongozi hao pamoja na kuwahamasisha watumishi washiriki michezo, wao wenyewe pia walishiriki michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, kuvuta kamba na mpira wa pete.

“Ni wajibu wa Viongozi mahali pa kazi kuwakumbusha watumishi kufanya mazoezi. Nawasihi, bonanza hili tulifanye kila inapowezekana” alisisitiza Prof. Turuka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi alisema kwamba akiwa kama kiongozi wa Wizara yenye dhamana ya michezo, anawakuwakumbusha watumishi umuhimu wa michezo.

[caption id="attachment_33809" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka,Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi wakikagua timu ya mpira wa pete kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri[/caption] [caption id="attachment_33810" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka akizungumza na timu za mpira wa pete kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limeandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo na limefanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33811" align="aligncenter" width="800"] Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka na akishiriki mazoezi ya mbio za polepole(jogging) na viongozi wengine wa Serikali wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma. Bonanza hilo limeandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na limefanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33812" align="aligncenter" width="800"] Timu ya Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakiongozwa na Kaimu katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Florens Turuka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza maalum la kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma.Bonanza hilo limefanyika katika Uwanja wa Jamhuri[/caption]

“Napenda kuwakumbusha umuhimu wa michezo kwa afya zetu, lakini pia michezo inaimarisha ushirikiano kati ya viongozi na watumishi”. Bi Mlawi.

Bonanza hilo lilianza saa 12:00 asubuhi kwa washiriki kukimbia mbio fupi kwa mwendo wa pole. Michezo mbalimbali pamoja na mazoezi ya viungo ilikuwepo katika kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi. Takribani wizara zote zote zilishiriki ikiwa ni pamoja na Tasisi chache.

Bonanza la michezo na mazoezi ya viungo lililoandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo limefana kiasi cha kumalizika likiwaacha washiriki wakiwa bado na kiu ya kuendelea na  michezo mbalimbali iliyofanyika katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi