Ndege ya tatu ya Bombadier Dash-8 Q-400 ikipigiwa saluti ya maji (Water Salute) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo Aprili 2, 2018
Ndege mpya ya Serikali aina ya Bombadier Dash-8 Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu April 2, 2018.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwaongoza Viongozi wengine wa Serikali kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege mpya ya Serikali aina ya Bombadier Dash-8 Q400 iliyowasili leo Jumatatu April 2, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier Dash-8 Q400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo Aprili 2, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye ndege ya tatu ya Bombadier Dash-8 Q-400 ilipoipokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo Aprili 2, 2018