Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bodi ya Filamu na Kamati ya Maudhui TCRA Kaeni Pamoja Muwekeke Uwiano Katika Maudhui – Waziri Mwakyembe
Feb 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na: Mwandishi Wetu

Bodi ya FilamuTanzania imeagizwa kukaa pamojana kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuangalia namna watakavykubaliana kuwa na uwiano sawa katika muda wa kuruhusu baadhi ya maudhui ya filamu na vipindi kuruhusiwa kurushwa au kuonyeshwa katika luninga na majumba ya sinema kulinga na matakwa ya sharia ili kulinda maadili ya mtanzania.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakembe alipokutana na wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania jana jijini Dar es Salaam.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa haiwezekani watu mkawa mnajenga nyumba moja alafu wakawa wanagombea fito moja, kuwa ni suala lisilo kubalika ni vyema waka kaa pamoja na kuja na kauli moja kwani lengo ni kuhakikisha maadili ya mtanzania hasa kijana ynalindwa.

“ Nyie Bodi ya Filamu mmepewa jukumu kubwa la kuhakikisha mnalinda maadili nautamaduni wa mtanzania, hivyo ninawaagiza ifikapo tarehe 1/6/2018 muwe mmekwisha kaa pamoja na wenzenu wa kamati ya maudhui ya TCRA ili mjadili na kukubaliana muda wa kuruhusu kuonyeshwa kwa filamu au vipindi katika luninga na majumba ya sinema kulingana na madaraja kama sheria inavyotaka,” alisema Mwakyembe.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi. Joyce Fissoo amemuhakikishia Waziri Mwakyembe kuwa utekelezaji wa agizo hilo utafanyika mara moja kwa kuwa jambo hilo limekuwa changamoto kwao katika kusimamia matakwa ya sheria ya filamu hali inayosababisha kuleta mkanganyiko kwa wateja wao.

“Mhe. Waziri suala hili limekuwa likitupa changamoto kubwa sana katika kusimamia matakwa ya sheria yetu ya filamu ya, hivyo nakuhakikishia agizo lako tutalitekeleza kwa wakati ili kumaliza sintofahamu hii ya muda mrefu,” alisema Fissoo.

Fissoo alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Filamu na kanuni zake inaainisha kuwa daraja la umri wa miaka 16, maudhui yake yanapaswa kuonyeshwa kuanzia saa sita usi wakati kwa mujibu wa TCRA umri huo huomuda wao ni kuanzia saa tatu usiku jambi linaloleta mkanganyiko.

Akisoma taarifa yautekelezaji wa Bodi ya Filamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Sylivester Sengerema amemuomba Waziri Mwakyembe akuongeza nguvu katika jitihada za kuhakikisha Sera ya Filamu nchini inapatikana jambo ambalo litakuwa suluhu ya mambo mengi yanayohusu tasnia hiyo na kuweka mazingira wezeshi katika usimamizi na uendeshaji wake.

Waziri Mwakyembe amefanya ziara yake ya kwanza katika Ofisi ya Bodi ya Filamu, na kasha kutmbelea baadhi ya wadau wa tasnia ya  Filamu kwakutembelea studi za Jason, Starline na Wanene amabao ni wadau wakubwa katika mendeleo ya filamu nchini na kuahidi ushirikiano kutoka serikalini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi