Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Biteko Ataka Soko la Madini Kufunguliwa Bunda
Dec 29, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Bunda,  Afisa Madini Mkazi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kuhakikisha wanafungua Soko la Madini wilayani  Bunda ili kuwarahisishia wachimbaji na  wafanyabiashara wa madini kupata huduma hiyo karibu.

Agizo hilo amelitoa leo Desemba 28, 2021 wakati akizungumza na wachimbaji katika eneo la Kinyambwiga lililopo Kata ya Guta wilayani Bunda mkoani Mara.

Dkt. Biteko amesema kuwa, haiwezekeni mchimbaji ana dhahabu yake mfukoni anaenda hadi Musoma kutafuta soko.

Amesema, ni lazima soko la madini lianzishwe Bunda ili watu wafanye biashara ya madini kwa urahisi.

"Natoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya, Afisa Madini na Katibu Tawala wa Mkoa ambaye kwa mujibu wa kanuni ya uanzishwaji wa masoko ya madini ndiye mwenye kutafuta eneo sahihi la kuweka soko la madini," ameongeza Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, bado kuna umbali mkubwa kutoka eneo la machimbo mpaka Bunda hivyo amewataka kianzishwe kituo kidogo cha kununua madini katika eneo la Kinyambwiga.

Amesema, eneo litaandaliwa kwa wafanyabiashara wa madini (Brokers) ili biashara yote ifanyike katika eneo hilo la wachimbaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi