Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bima ya Afya kwa Wote Kuboresha Huduma za Nchini
Nov 01, 2023
Bima ya Afya kwa Wote Kuboresha Huduma za Nchini
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha bungeni Muswada wa Kutunga Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Na. 8 wa mwaka 2022 bungeni jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu - Dodoma

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Mfumo wa Bima ya Afya ndio mfumo bora, rahisi na endelevu duniani katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote.

Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo wakati akiwasilisha bungeni Muswada wa Kutunga Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Na. 8 wa mwaka 2022.

“Lengo la kutungwa kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa  wote kupitia mfumo wa bima ya afya kwa raia na wakazi wote.  

Akifafanua kuhusu vifungu vya Muswaada huo, Mhe. Ummy amesema kuwa Kifungu cha 29 cha Muswada kinaruhusu skimu za bima ya afya za umma na binafsi kufanya uwekezaji kwa lengo la kukuza mtaji na kuimarisha uendelevu wake.  

Aidha, Kifungu cha 35 kinaweka utaratibu wa kushughulikia madai ya skimu za Bima ya afya ambapo mahakama ina uwezo wa kuamuru ulipwaji wa fidia iwapo kosa litathibitika kutendwa na mwanachama au mtu yoyote.

Ameeleza kuwa athari za kutotungwa kwa Sheria hiyo ni kubwa, wananchi asilimia 85 watakuwa nje ya mfumo wa bima ya afya, wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akieleza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita, Mhe. Ummy amesema: “Tunamshukuru na Kumpongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuhakikisha kuwa watu wasio na uwezo wanapata huduma bora za afya bila kikwazo chochote.

Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake shupavu, upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya imeongezeka kutoka asilimia 62 mwezi Agosti, 2022 hadi asilimia 73 Agosti 2023,” ameeleza Mhe. Ummy.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi