Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 3 Zakopeshwa Kuwezesha Miradi ya Vijana
Aug 11, 2023
Bilioni 3 Zakopeshwa Kuwezesha Miradi ya Vijana
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akizungumza wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Vijana kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, lililofanyika katika ukumbi wa Mabele tarehe 11 Agosti, 2023 jijini Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi  ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye  Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema katika mwaka wa fedha 2022/23,  miradi 149 iliyoibuliwa na vijana imepata mikopo ya Sh.ilingi bilioni 3.2 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Vijana Duniani (UNFPA), Mark Schreiner akichangia jambo wakati wa kongamano hilo.



Akifungua Kongamano la Kitaifa la Vijana katika kuelekea siku ya kimataifa ya vijana Agosti 11, 2023 jijini Dodoma, Prof. Katundu amesema miradi hiyo ni ya kwenye  sekta ya kilimo, viwanda, usafirishaji na  biashara.

Sehemu ya Vijana pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu waliohudhuria kongamano hilo.


Katibu Mkuu huyo amesema kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15-35 ni asilimia 34.5 hivyo wanatakiwa kujengewa uwezo wa kiuchumi.

Naye, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic, amesema kuna umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kiuchumi kwa kuwa inasaidia kuinua Pato la Taifa husika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi