Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

BASHE Apongeza Juhusi za Serikali ya Awamu ya Tano
Mar 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo upatikanaji wa huduma za kijamii katika Jimbo la Nzega Mjini.

Kwa mujibu wa Bashe amesema kuwa, Maendeleo ya watu ni kugusa maisha ya watu na moja ya njia hizo ni kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii, mathalani upatikanaji wa huduma bora za afya.

Mheshimiwa Bashe amesema kuwa, Rais Magufuli ametekeleza kwa vitendo ujenzi na ukarabati mkubwa wa upanuzi wa Kituo cha Afya cha Zogolo na sasa kina hadhi ya hospitali ya kisasa na ya kuigwa.

“Hii ilikuwa ni ndoto yangu mwaka 2015 wakati wa kampeni kuhakikisha Kituo cha Afya cha Zogolo kinakuwa na hadhi ya hospitali kubwa na ya kisasa ili kuweza kuhudumia Wananchi wengi ndani ya Jimbo la Nzega Mjini”

“Mpaka hapa, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini, Serikali Kuu pamoja na Watalaam wa Halmashauri ya Mji wa Nzega lakini kipekee kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli” amefafanua Mhe. Bashe.

Aidha, Mhe. Bashe ameongeza kuwa kupitia mradi wa ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya cha Zogolo kuwa na hadhi ya hospitali, Jimbo la Nzega Mjini limefanikiwa kujenga wodi ya wagonjwa wa nje (OPD) ya kisasa, Majengo ya upasuaji, majengo ya wagonjwa mahututi, jengo kubwa la mochwari ya kisasa, maabara ya kisasa, wodi kubwa ya kisasa ya wakina mama na watoto pamoja na nyumba za kisasa za watumishi wa hospitali.

Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za kijamii kwa kuboresha vituo vya afya, kutoa elimu bila malipo na kuongeza bajeti ya ununuzi wa madawa

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi