[caption id="attachment_13837" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimsisitizia jambo Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock walipokuwa wakiagana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.[/caption]
Mwandishi wetu – Singida.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock leo amefanya ziara mkoani Singida na kuahidi kuangalia namna ya kufadhili ujenzi wa mabwawa ili yaweze kusaidia kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea pekee.
Mhe. Sherlock amewatembelea wanufaika wa misaada wanayotoa katika Vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi vya Siuyu na Faraja mara baada ya yeye na mabalozi wengine kumaliza shughuli maalumu bungeni Dodoma.
[caption id="attachment_13840" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiagana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock, nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.[/caption]Ameeleza kuwa amefurahishwa na hali ya hewa ya Mkoa wa Singida huku akisema kuwa uwepo wa barabara nzuri umerahisisha safari yake Mkoani humo ambapo ni jirani na makao makuu ya nchi.
Mhe. Sherlock ameongeza kuwa anautazama mkoa wa Singida katika sura ya maendeleo zaidi kutokana na fursa zilizopo huku akiahidi kuanzisha miradi itakayosaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la alizeti linalozalishwa kwa wingi Singida.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema ameupokea ujio wa balozi huyo kwa furaha kubwa kwa kuwa hiyo ni ishara ya kufunguliwa zaidi kwa milango ya mahusiano mazuri.
Dkt. Nchimbi amesema moja ya faida ya Singida kuwa jirani na makao makuu ni kupata wageni ambao wanaitazama Singida kwa mtazamo wa maendeleo zaidi na ishara Singida itapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi.
[caption id="attachment_13841" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati), Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi (kulia) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.[/caption]Amesema kilimo cha umwagiliaji kina tija zaidi kuliko kutegemea mvua pekee ambapo Singida inajipanga kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula nchini huku ikiwa na lengo la kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya makao makuu ya nchi ambayo maeneo mengi yatakuwa na shughuli za kiofisi zaidi.
Dkt. Nchimbi amesisitiza Mkoa wa Singida hauna njaa, sio masikini na wala sio kame na wananchi wa Singida wamejipanga kutumia fursa zote zinazojitokeza kwa ajili la kukuza uchumi.
Aidha amewataka wananchi wa Singida kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuwa washiriki wakubwa katika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda.