Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Azma ya Serikali ni Kuwapatia Watanzania Nishati ya Uhakika - Dkt. Biteko
Sep 04, 2023
Azma ya Serikali  ni Kuwapatia Watanzania Nishati ya Uhakika - Dkt. Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko akizungumza na watumishi wa Wizara ya Nishati mara baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika wizara hiyo.
Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amewataka Watumishi wa Wizara ya Nishati  kufanya kazi kwa weledi na ubunifu kwa lengo la kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwapatia wananchi nishati ya uhakika.

Ameyasema hayo  leo Septemba 4, 2023 jijini Dodoma  wakati wa hafla ya kumpokea iliyofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo.

“Kazi iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha  Watanzania wanapata huduma bora ya nishati kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tayari kazi kubwa imeshafanyika  katika sekta hii, kazi yetu kuanzia sasa ni kuendeleza mazuri yaliyokwishafanyika katika sekta yetu,” alisisitiza Dkt . Biteko

Akifafanua amesema, kazi kubwa ya Wizara hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata nishati ya uhakika kwa kuongeza kasi ya utendaji kwenye sekta.

Aidha, Mhe. Biteko amewahakikishia watumishi wa Wizara hiyo kuwa jukumu lake kwa kushirikiana nao ni kuweka alama katika sekta hiyo kwa kutimiza malengo yaliyowekwa katika sekta.

Sanjari na hilo, Mhe. Dkt.  Biteko amesema kuwa dhamira yake ni kuwafanya watumishi wa Wizara hiyo wafanye kazi kwa weledi na katika mazingira mazuri ili kuleta tija.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Judith Kapinga amewahakikishia Watumishi wa Wizara hiyo ushirikianao na kuwataka kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo.

Aliwashukuru watumishi wote kwa ushirikiano walioanza kuutoa  kwake katika kutekeleza majukumu yake kama Naibu Waziri na kuahidi kutoa ushirikiano na kufuata miongozo itakayotolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Biteko.

Sekta ya nishati ni muhimili katika ujenzi wa Taifa kikiwa kichocheo cha ustawi wa wananchi na sekta nyingine kama viwanda, madini, ujenzi na nyingine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi