Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Aweso Akagua Maendeleo Utekelezaji wa Mradi wa Maji Longido
Dec 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_24140" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo wakitoka kukagua chanzo cha maji cha Mto Simba kilichopo wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro kitakachotumiwa na mradi wa Longido.[/caption]

Na.Mwandishi Wetu, Arusha.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ametembelea mradi wa maji wa Longido, katika Jiji la Arusha kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wake.

Naibu Waziri Aweso ameweza kujionea maendeleo ya mradi huo kwa kukagua ujenzi wa chanzo cha maji cha Mto Simba, kilichopo wilayani Siha, katika mkoa wa Kilimanjaro, ulazaji wa mabomba yenye umbali wa kilomita 65 mpaka Longido na ujenzi wa tenki la maji la lita 450,000.

‘‘Nimekuja Longido kuangalia hali ya utekelezaji wa mradi huu, lakini sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wake. Na mimi kama msimamizi wa miradi ya maji, hatuna budi  kuchukua hatua sahihi ili mradi huu ukamilike kwa wakati’’, alisema Aweso.

[caption id="attachment_24141" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya (kushoto), Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo wakiangalia hatua ya ulazaji wa mabomba ya mradi wa Longido, mkoani Arusha.[/caption] [caption id="attachment_24142" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo katika sehemu ya mradi wa Longido, mkoani Arusha.[/caption] [caption id="attachment_24143" align="aligncenter" width="750"] Ujenzi wa tenki la mradi wa Longido ukiendelea, mkoani Arusha.[/caption]

‘‘Nitazungumza na Katibu Mkuu aweze kufika hapa, ili kutatua changamoto za mradi huu na kukamilika. Ni lazima mradi huu ukamilike na wananchi wa Longido waanze kupata maji na kumaliza adha wanayoipata sasa kama Serikali ilivyoahidi. Kuna haja ya wakandarasi wanaofanya kazi hii kuongeza kasi ili wamalize kazi waliyopewa.’’, alisisitiza Naibu Waziri.

Wakati huo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongollo amesema kuwa yeye pamoja na uongozi wa wilaya hiyo utahakikisha unasimamia ipasavyo ujenzi wa mradi huo na ikibidi kuchukua hatua stahiki kwa mkandarasi atakayekwamisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Mradi wa maji wa Longido unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusimamiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na fedha za ndani za Serikali unaotarajiwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 15.8 na kukamilika Mei, 2018.

         

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi